KAHAMA,KIBAHA,GEITA MUDA WOWOTE KUPANDISHWA HADHI NA KUWA MANISPAA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Kutoka Jijini Dodoma.

Bunge limeelezwa kuwa ,Serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi halmashauri 3 hapa nchini kutokana na kukidhi vigezo vya mapato kujitosheleza. 


Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mhe.Seleman Jafo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Msalala Kahama Ezekiel Maige aliyehoji,lini mji wa Kahama utapandisha kuwa hadhi kuwa Manispaa baada ya kutimiza vigezo vya mapato kujitosheleza  pamoja na Isaka kupandishwa hadhi ya Mji. 


Akijibu Swali hilo,Waziri wa TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema Serikali inatambua maeneo matatu hapa nchini ambayo serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi kuwa Manispaa kutokana na kukidhi vigezo vya kujitosheleza kimapato. 


Mhe.Jafo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani na Halmashauri ya  mji wa Geita mkoani Geita na muda wowote kuanzia sasa maeneo hayo yatapandishwa hadhi kuwa Manispaa pindi mchakato utakapokamilika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527