COSTECH YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KURIPOTI TAARIFA ZA MATOKEO YA UTAFITI

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuripoti taarifa za matokeo ya tafiti zinaofanywa na taasisi mbalimbali ili wananchi waweze kupata taarifa.

Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Bakari Msangi kwenye Mafunzo yaliyohusisha wana habari,Watafiti na wawakilishi kutoka SIDO na VETA yanayofanyika katika ukumbi wa VETA Mtwara.


Dkt. Msangi ameongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza zaidi habari za Michezo,Burudani na Siasa kuliko Habari za Utafiti ambazo zingesaidia wananchi kupata Elimu kuhusu mambo mbalimbali yatokanayo na tafiti ikiwemo kilimo

Amefafanua kuwa ni vema kuripoti matukio na matokeo ya Tafiti kwa lugha rahisi na zinazoeleweka kwa wananchi kutokana na mahitaji husika ya habari

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza jana yameandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) lenye jukumu la kuhamasisha, kuratibu, kuhifadhi, kusambaza na kuendeleza tafiti chini.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Bakari Msangi akifungua mafunzo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527