WILLIAM BUNDALA AFARIKI DUNIA,AZIKWA KIJIJINI KWAO ULOWA USHETU | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, May 26, 2019

WILLIAM BUNDALA AFARIKI DUNIA,AZIKWA KIJIJINI KWAO ULOWA USHETU

  Malunde       Sunday, May 26, 2019

Babu wa Mtangazaji maarufu nchini William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K, Mzee William Bundala Ndabihizye (89) amefariki dunia.


Mzee Bundala amefariki dunia juzi majira ya saba mchana kufuatia kuugua ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.

Kwa mujibu wa Mjukuu wake William Bundala (Kijukuu cha bibi K) ambaye sasa anafanya kazi Kahama Fm na mmliki wa Kijukuu blog ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio Free Africa, ameiambia Malunde 1 blog kuwa babu yake, mzee William Bundala Ndabihizye alianza kuugua tangu tarehe 15/5/2019 na kufariki dunia Mei 24,2019.

Mzee William Bundala Ndabihizye ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la ardhi na mwenyekiti wa kitongoji cha Kangeme B kijiji cha Kangeme kata ya Ulowa kwa kipindi cha miaka 20, amezikwa kijijini kwao Kangeme kata ya Ulowa halmshauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.

Alizaliwa mwaka 1930 katika kijiji cha Ubagwe,ameacha mjane,watoto 9,wajukuu 33,vitukuu 10.
Mzee William Bundala enzi za uhai wake
William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K akiwa kwenye kaburi la Babu yake Mzee William Bundala Ndabihizye.
William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K akiaga mwili wa Babu yake Mzee William Bundala.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Mzee William Bundala.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post