URUSI KUUNDA INTERNET YAKE YA PEKEE

Bunge la Urusi limepitisha muswada ambao ukiwa sheria basi Taifa hilo lenye Watu zaidi ya M.140 litaunda INTERNET yake peke yake na kuachana na inayotumika duniani.


Muswada huo uliopitishwa kwa kura nyingi za wabunge 307 huku 68 wakiupinga, utawasilishwa katika Bunge Kuu la Urusi ili kuidhinishwa na kisha kuwasilishwa kwa Rais Vladmir Putin kutia sahihi ili kuufanya sheria kamili na kuanza kutekelezwa Novemba, mosi.

Sheria hiyo itawezesha Serikali ya Urusi kubuni miundombinu yake binafsi ya Intaneti na kuweza kusalia mtandaoni hata kukitokea dharura ya taifa lolote kujaribu kuuzima.

Mmoja wa waandishi wa muswada huo, Andrei Klishas aliliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DW) kuwa hawana shaka Marekani ina uwezo wa kiufundi wa kuizimia Urusi huduma za intaneti wakati wowote wakipenda, hivyo wanajiandaa kiufundi kuhakikisha wanajilinda dhidi ya mashambulizi kama hayo.

Hadi sasa maswala ya kiufundi ya namna miundombinu hiyo itakuwa hayajakuwa bayana, lakini taasisi kuu ya mawasiliano ya Urusi – Roskomnadzor ndiyo itakuwa kituo kikuu cha kufuatilia na itasimamia intaneti hiyo kukitokea mashambulizi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post