TAKUKURU NJOMBE YACHUNGUZA MRADI WA MABILIONI YA PESA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 16, 2019

TAKUKURU NJOMBE YACHUNGUZA MRADI WA MABILIONI YA PESA

  Malunde       Tuesday, April 16, 2019
Na Amiri kilagalila, Njombe.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe inaendelea na uchunguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Njombe mjini ambacho kimeshindwa kukamilika kwa wakati na kuchukua zaidi ya miaka 6 mpaka sasa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoani Njombe , Bw Charles Mulebya wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.

"TAKUKURU mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu (2019) tulianza kufanya uchunguzi juu ya ujenzi wa stendi kuu ya mabasi inayoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Njombe, kufuatia taarifa ya ukaguzi uliofanywa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na kuibua ubadhilifu katika ujenzi huo.” Alisema Bw Mulebya.

Aidha, Bw Mulebya alisema kuwa kutokana na uchunguzi wanaoufanya mpaka Sasa wamefikia katika hatua nzuri na  karibuni utakamilika.

“Ujenzi huu utagharimu shilingi Bil 9.7 hadi kukamilika kwake na uchunguzi upo kwenye hatua nzuri za kukamilika, uchunguzi unafanyika kwa umakini mkubwa ili yeyote aliyehusika akutane na mkono wa sheria kwa kusababisha ucheleweshwaji wa kituo hicho pamoja na ubadhilifu wa fedha ulioibuliwa hivi karibuni.” ameongeza Bw Mulebya.

Mbali na hivyo, Kaimu huyo amebainisha kuwa uchunguzi wa majalada ya mwanzo umebaini makosa chini ya manunuzi ya umma na kanuni zake za mwaka 2013 na mara baada ya kukamilika majalada yatapelekwa makao makuu kwa hatua zaidi.

Katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  iliyofanyika kwa siku tatu mkoani Njombe, Rais alimuagiza mkurugenzi na mkandarasi wa kituo hicho cha mabasi mjini Njombe kuhakikisha mpaka mei 5  kimekamilika na kuanza kutumiwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post