TAKUKURU DODOMA YAOKOA MILIONI 152....MILIONI 900 ZINACHUNGUZWA


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dodoma imesema inachunguza ufisadi wa shilingi Milioni 900  baada ya kuwa na viashiria vya rushwa katika miradi mbalimbali.Pia taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh152.3 milioni ambazo zingelipwa kwa wakandarasi ambao ufuatiliaji wa ukaguzi wa miradi ya maji umebaini hawakutimiza majukumu yao ipasavyo.

Hayo yamebainishwa jana  mkoani Dodoma na kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, mkoa wa Dodoma Sosteth kibwengo wakati akitoa taarifa ya robo ya mwaka kwa wanahabari.

Ambapo alisema kwa robo ya mwaka taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi  milioni 152.3, zilizokuwa zilipwe kwa wakandarasi ambao hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi hiyo  pia imemtaka mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited, inayojenga kituo cha afya Mima kilichopo Wilayani Mpwapwa mkoani hapa kulipoti katika ofisi ya zake zilizopo wilayani humo kwa mahojiano.

Vile vile alibainisha kuwa katika kipindi husika, TAKUKURU ilipokea jumla ya taarifa 96 za rushwa na makosa yahusianayo ambapo sekta  ziliongoza kwa tuhuma ni;

Serikali za mitaa (25%), Ardhi (17%), Elimu (16%), Afya (8%), Maji, Ujenzi na Mahakama (kila moja asilimia 7), na Polisi (6%), taarifa hizo zilifanyiwa kazi kwa njia mbalimbali na majalada nane (8) ya uchunguzi yalikamilika ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.5 ya majalada yaliyokamilika kwa kipindi hicho mwaka 2018.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post