SPIKA NDUGAI : BUNGE HALITAFANYA KAZI NA MTU ANAYEITWA PROF. MUSSA ASSAD NA SI OFISI YA CAG



Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwamba, Bunge limekataa kufanya kazi na mtu ambaye ni Profesa Mussa Assad, na siyo ofisi ya CAG, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyonukuu.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni.

"Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Prof. Mussa Juma Assad, halijakataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG, sisi kama Bunge hatujawahi kukataa kufanya kazi na taasisi yoyote" Amesema Spika Job Ndugai

Juzi, Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527