GODBLESS LEMA AFUNGUKA BAADA YA KUPEWA ADHABU YA KUTOHUDHURIA MIKUTANO MITATU YA BUNGE


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema adhabu aliyopewa na Bunge ya kutohudhuria mikutano mitatu ni kitu kinachompa nguvu kwenye mapambano dhidi ya kudai haki na kamwe hatanyamaza hata kama adhabu yake itakuwa ni mauti.


Katika ujumbe ambao ameuandika katika akaunti yake ya Twittwer, Lema amesena, “Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka Januari 2020. Moyo wangu una amani sana, kwani mahusiano yangu na HAKI yanaendelea kuimarika zaidi.Nawatakia Wabunge wenzangu kazi njema katika wajibu huu, sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa ni mauti.”

“Msiogope. Mungu aliyetupa macho sio kipofu kwamba haoni, Mungu aliyetupa masikio sio kiziwi kwamba hasikii.Yeye ni Mungu asiyekuwa na msongo wa mawazo kama sisi. Siku imekaribia sana kwa kila mtu kulipa kwa kadri alivyopanda.” Ameandika Godbless Lema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527