Saturday, April 13, 2019

SIMBA YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA...YALALA NA MABAO 4 YA TP MAZEMBE

  Malunde       Saturday, April 13, 2019

Simba imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo Jumamosi kuchapwa mabao 4-1 na TP Mazembe ya DR Congo.


Huo unakuwa mwendelezo wa Simba kupoteza mechi za ugenini kwani tangu hatua ya makundi walipoteza mechi tatu kwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita ya Congo na Al Ahly ya Misri na mabao 2-0 kutoka kwa JS Saoura ya Algeria hivyo katika mchezo minne ya ugenini imeruhusu mabao 16.

Katika mchezo huo wa Robo fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade TP Mazembe Lubumbashi DR Congo Simba ilionekana kuzididwa muda mwingi wa mchezo huku safu ya ulinzi ikionyesha udhaifu mkubwa.

Licha ya Simba kuanza kufunga bao dakika ya pili kupitia kwa Emmanuel Okwi lakini haikuwasaidia kuepuka kipigo hicho kikubwa na kuendeleza rekodi yao mbovu ya kupoteza mechi za ugenini tangu hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya pili tu ya mchezo lililofungwa na Emmanuel Okwi ambaye alimalizia pasi safi ya Haruna Niyonzima.

Kuingia kwa bao hilo kuliwanyong'onyesha mashabiki wa TP ambao walibaki wameduaaa na kuacha kushangilia.

Dakika ya 21 Kabaso Chongo aliisawazishia TP Mazembe bao kwa shuti la kawaida baada ya wachezaji wa Simba kujichanganya kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Rainford Kalaba.

Meshack Elia aliipatia TP Mazembe bao la pili dakika ya 38 baada ya mabeki wa Simba, Juuko Murshid na Zama Coulibaly kujichanganya wakati wakiokoa kabla ya mkongwe Tresor Mputu kuipatia timu yake bao la tatu dakika ya 62 kwa shuti kali nma kufikisha mabao matano katika mashindano hayo.

TP Mazembe hawakulizika kwani waliendelea kufanya mashabulizi mengi golini jkwa Simba na kufanikiwa kuandika bao la nne dakika ya 75 kupitia kwa
Jackson Muleka ambaye naye amefikisha mabao matano sawa na Mputu na Clatous Chama wa Simba.

 Na Oliver Albert - Mwanaspoti
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post