MTOTO AMPA KICHAPO BABA YAKE KISA KAMKATAZA KUMVIZIA BINTI WA JIRANI....AUA BABA WA BINTI

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Baragoi, kaunti ya Samburu, nchini Kenya amemvamia na kumtandika babake baada ya kudaiwa kumuonya dhidi ya kumvizia na kumchumbia binti wa jirani yao.

Mvulana huyo alijawa na hasira baada ya babake kumuonya dhidi ya kumvizia na kumchumbia mtoto wa jirani yake  na baada ya kumpa kichapo babaake, mvulana huyo alitoroka.

 Inadaiwa kuwa, kabla ya kumpa babake kichapo cha mbwa koko, mwanafunzi huyo awali alikuwa ametekeleza mauaji ya baba wa binti huyo baada ya kumdunga kisu.

 Kulingana na Citizen, mtuhumiwa huyo ambaye alitoweka baada ya tukio hilo, alipandwa na mori baada ya babake kumkanya dhidi ya nia yake ya kumvizia binti huyo. 

Chifu wa eneo hilo Sammy Lothuru alisema kuwa, binti huyo alikuwa amekataa jaribio la mvulana huyo kumchumbia na hata akamripoti kwa babake aliyechukua hatua ya kumuonya dhidi ya jaribilio hilo.

 "Mshukiwa alijaribu kumfichulia binti huyo kuhusu hisia zake, lakini alikataa na hata akamripoti kwa babake. Babaake msichana alimshtaki mvulana huyo kwa babaake, ambaye alimuonya. 

Hata hivyo mtuhumiwa alipandwa na hasira na kumpa babake kichapo kabla ya kutoweka nyumbani kwao," Lothuru alisema. 

Kwa sasa, maafisa wa polisi wanamsaka mvulana huyo wa miaka 17. 
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post