Wednesday, April 3, 2019

MECHI YA SIMBA NA JKT YAAHIRISHWA

  Malunde       Wednesday, April 3, 2019

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa upigwe katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro, umeahirishwa kutokana na mvua.

Mvua kubwa iliyonyesha mchana mjini Morogoro, imesababisha Uwanja wa Jamhuri kujaa maji kiasi cha mpira kushindwa kudunda. Baada ya kusubiri kwa nusu saa, wasimamizi wa mechi wakaamua kuahirisha na kuahidi kuupangia ratiba nyingine.

Charles Mwakambaya ambaye ni Katibu wa chama cha soka mkoani Morogoro na msimamizi wa TFF kituo cha Morogoro, akizungumza baada ya mchezo kuahirishwa amesema kuwa hawatoweza kuipangia ratiba Simba kucheza kesho kwa sababu ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, Jumamosi dhidi ya TP Mazembe.

"Hatuwezi kusema kuwa mchezo uchezwe kesho kwa sababu Simba ina ratiba ya mchezo wa TP Mazembe Jumamosi hii, kwahiyo wakicheza kesho tutakuwa tumewanyima masaa 48 ya kujiandaa dhidi ya mchezo mwingine", amesema Mwakambaya.

Kuhusu mashabiki ambao walishalipia tiketi zao, Mwakambaya amesema kuwa hela hazitorudishwa lakini utafanyika utaratibu mzuri na mambo yatakuwa sawa kwa mashabiki hao.

Simba sasa itarejea Jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ambao inaelezwa kuwa wameshatua nchini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post