RAIS MAGUFULI AWAONYA WANAOSAMBAZA PEMBEJEO HEWA


Rais Magufuli amekemea vikali watu wanaosambaza pembejeo hewa na amewataka waache kufanya hivyo kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 11, kabla ya hajafungua barabara ya Mafinga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7 katika eneo la mtewele na uwanja wa Polisi –Makambako mkoani Njombe.

“Mtu anadai amesambaza magunia kadhaa ya pembejeo wakati hayapo, hatuwezi tukaendelea na nchi yenye hewa kwa sababu hatuwezi kushiba hewa.

“Nilipoingia madarakani niliahidi nitakuwa daktari wa kutumbua majipu zikiwemo hizi hewa ili fedha halali zitumike katika masuala mengine halali, ninajua wapo waliopata pembejeo za haki na tukishamaliza ufuatiliaji wa pembejeo watalipwa,” amesema.

Aidha amewapongeza wakazi wa Mkoa huo kwa ujenzi mzuri wa nyumba ambapo ameitaka mikoa mingine kuiga mfano huo kwa kujenga nyumba nzuri na za kisasa.

“Tangu nimeingia Njombe nimeona nyumba zilizojengwa ni tofauti na nyumba zilizonyengwa huko kwetu kwani hakuna nyumba ya majani zote ni za bati na zimejengwa kwa matofali ya kuchoma ninafikiri mikoa mingine ambayo haijabadilika katika ujenzi wa nyumba waje wajifunze huku,” amesema Dk Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post