Picha : VIJANA WA JUMUIYA YA WAISLAM WA AHMADIYYA SHINYANGA WACHANGIA DAMU NA KUFANYA USAFI ZAHANATI YA NHELEGANI

Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga (Ahmadiyya Muslim Jamaat Mkoa wa Shinyanga) wakiongozwa na vijana wa Jumuiya hiyo wamejitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto katika Zahanati ya Nhelegani iliyopo katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga. 


Zoezi hilo la uchangiaji damu limefanyika leo Alhamis Aprili 11,2019 ambapo mbali na kuchangia damu vijana hao wamesafisha mazingira katika zahanati hiyo kwa kufyeka nyasi na kuzoa taka. 

Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka alisema wameamua kuchangia damu ili kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia kufanya usafi ili kuweka mazingira ya zanahati ya Nhelegani kuwa salama. 

“Tumehamasishana kufanya shughuli hizi kwa mikono yetu,hali hii ya kujitolea inajulikana kwa jina la‘Waqar Amal’ ikiwa na maana ya kujitolea kusaidia kwa mikono yako mwenyewe,utoke jasho mwenyewe, hili ni zoezi endelevu tumekuwa tukijitolea katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na maeneo mengine duniani”,alieleza Sheikh Mgeleka. 

“Tunafanya popote na hatubagui kwa ajili ya manufaa ya viumbe vya Mwenyezi Mungu na hii ni sehemu ya mafundisho ya dini Tukufu ya Islam,malipo ya jasho letu ni mbele ya Mungu na haya ndiyo mafundisho muhimu ambayo daima tunatakiwa kukumbushana kwa ajili ya kusaidia viumbe wenzetu,pia tumefundishwa kuwa kujitolea ni heshima”,alisema Sheikh Mgeleka. 

Naye Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko alisema zoezi la kuchangia damu ni huduma kwa viumbe ijulikanayo kwa jina la ‘Khidmatil Khalqi’ ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu ya Ahmadiyya ya ‘Upendo kwa wote bila chuki kwa yeyote’

“Zoezi hili limeshirikisha vijana wa Ahmadiyya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Masheikh wa matawi mbalimbali wakionesha mfano kwa waumini tunaowaongoza, hili ni agizo la Kiongozi wetu Mtukufu Duniani Hazrat Mirza Masroor A.T.B.A Khalifatul Masihi wa tano kusaidia viumbe wenzetu”,alisema Sheikh Gesonko. 

“Tunatoa huduma kwa yeyote aliyepata shida ili apate uhai,tumeleta huduma hii kwenye zahanati inayosimamiwa na serikali kwa sababu serikali ndiyo wanahusika na majanga na huduma mbalimbali za binadamu hasa afya,na tumekuwa tukichangia damu hata kwenye mikutano yetu mikuu mwezi Septemba kila mwaka”,alisema Sheikh Gesonko.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Devotha Omary (kushoto) akiandika jina la Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko (wa pili kushoto mwenye kanzu ya bluu) baada ya kumpima wingi  wa damu wakati wa zoezi la utoaji damu katika Zahanati ya Nhelegani katika Manispa ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka(kulia) akipimwa presha wakati wa zoezi la uchangiaji damu.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko akitoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya mama na mtoto na watu wengine wenye uhitaji wa damu.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Lucy Biseko akimhudumia Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko baada ya kumaliza kutoa damu.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Lucy Biseko akimwandaa Mwenyekiti wa Vijana wa  Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Abdulghani Msimba ili atoe damu.
Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka akitoa damu
Mganga katika zahanati ya Nhelegani,Johanes Barnabas akiendelea na zoezi la kuwapima presha vijana wa Ahmadiyya waliojitolea kuchangia damu.
 Vijana wa Ahmadiyya wakijitolea kuchangia damu.
Zoezi la kuchangia damu likiendelea.
Sehemu ya damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga na Wataalamu wa Maabara wakiangalia damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko akionesha damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakitoka katika wodi ya wazazi katika zahanati ya Nhelegani kutoa zawadi ya sabuni za kufulia.
Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka akitoa zawadi ya soda kwa wagonjwa katika zahanati ya Nhelegani.
Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka,Mwenyekiti wa Vijana wa  Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Abdulghani Msimba na Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko wakitoa zawadi ya soda,maji na sabuni kwa wagonjwa katika zahanati ya Nhelegani.
Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakifyeka nyasi katika zahanati ya Nhelegani.
Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakiendelea kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.
Vijana wakiendelea na usafi.
Baada ya kumaliza kufanya usafi viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakiondoka eneo la zahanati ya Nhelegani.
Picha ya kumbukumbu : Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.
Picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.
Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakisali na kufanya ibada ikiongozwa naMwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka baada ya kumaliza kchangia damu na kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post