RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KWA WAKURUGENZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao watanaoesha nia kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali, kununua zao la korosho kwa bei elekezi ya shilini 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa korosho.


 Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Mtwara kuelekea Newala na Masasi, ambapo amesema serikali haiwezi kuamua kuwasaidia wananchi halafu Halmashauri ijitokeze kutaka ushuru.
 


"Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima".
 

"Haiwezi Serikali imepanga bei ya korosho 3300, halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, mkitaka ushuru msimamie vizuri bei ya korosho, siwezi nikakusanya hela mikoa mingine nije niwalipe nyinyi."Amesema Rais Magufuli


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527