RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3530


Katika kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Aprili 26, 2019, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa  msamaha kwa wafungwa ambapo kati ya waliopewa msamaha ni pamoja na wafungwa walioingia gerezani kabla ya machi 15, 2019.


Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530  ambapo wafungwa 722 wataachiliwa huru siku ya leo April 26, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Meja Jenerali Jacob G Kingu, imeeleza kwamba wafungwa 2808  watabaki gerezani kumalizia kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.

Wafungwa wengine waliobahatika msamaha huo ni pamoja na na wale wanaougua magonjwa kama Ukimwi, Kansa na Kifua kikuu ambapo watathibitishwa na Jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu Mkoa au Wilaya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527