RAIS MAGUFULI AAGIZA TCRA KUTOWABUGHUDHI WANANCHI KUSAJILI UPYA LAINI ZA SIMU KWA KITAMBULISHO CHA NIDA


Rais Magufuli, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA, kutowabughudhi watu ambao hawana vitambulisho vya taifa, katika zoezi ambalo limepanga kuanza tarehe 01, Mei mwaka huu.

Rais ametoa kauli hiyo leo wakati, akizungumza na wananchi wa Mbeya ambapo amesema kwamba zoezi hilo haliwezi kufanyika kama ilivyopangwa na TCRA kwa kuwa sio watu wote wanaomiliki simu wana Vitambulisho vya Taifa.

"TCRA wamesema watu wasajili simu kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa kwa 'logic' ya kawaida Watanzania waliopata vitambulisho ni milioni 14, ukisema mpaka vitambusho vya Taifa ndo wapate usajili ni kuwaeleza watanzania milioni 24 wasiwe  na simu. Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani", amesema JPM.

Rais amezitaka Mamlaka zinazohusika kuendelea na usajili wa laini kwa watu wenye vitambulisho tu, huku NIDA wakiendelea kusajili Wananchi ili kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.

"Ninawaambia TCRA na Wizara inayohusika jambo wanalolifanya ni zuri sana lakini waanze na wale milioni 14 walio na vitambulisho vya Taifa na zoezi la kusajili liende mpaka Desemba, ili liendane sawa na utoaji wa vitambulisho vya taifa", ameoongeza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post