Utafiti : WANASAYANSI 'WAFUFUA NGURUWE' WALIOKUFA

Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kufufua ubongo wa nguruwe kwa saa nne baada ya mnyama hayo kuchinjwa.


Japo uvumbuzi huo huenda ukazua mjadala kuhusu maana halisi ya tofauti kati ya uhai na kifo unafungua ukurasa mpya katika uchunguza wa magonjwa kama vile Alzheimer.

Utafiti huu mpya umebaini kuwa baadhi ya sehemu ya ubongo inaweza kufufuliwa ikiwa seli za ubongo zianaweza kusitishwa kufa.

Matokeo ya utafiti huu wa kushangaza inakinzana madai kuwa ubongo huacha kufanya kazi dakika chache baada ya usabazaji wa damu mwilini kukatizwa.

Utafiti ulivyofanywa?

Ubongo wa nguruwe 32 zilitumiwa kwa utafiti huu.

Saa nne baadae viungo hivyo vilirutubishwa kupitia mtambo maalum uliobuniwa na kundi la wanasayansi kutoka Chuo Kikuu Yale.

Mtambo huo ulitumiwa kuiga mapigo ya moyo na kuingiza mchanganyiko wa dawa ambayo pia imebeba oksijeni ili kupunguza au kugeuza kifo cha seli za ubongo.

Ubongo ulipewa muda wa saa sita kurejelea hali yake ya kawaida.
Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Nature, umeonesha kupungua kwa kifo cha seli za ubongo na kufanya kazi upya kwa mishipa ya damu na shughuli kiasi ya ubongo uliyopata uhai.

Watafiti waligundua kuwa seli ya ubongo ukiimarishwa unaweza kuwasiliana na sehemu nyingine ya mwili.

Ubongo ulionesha uwezo wa kupokea tiba na pia kutumia kiwango sawa cha oksijeni ya ubongo ulio hai.

Wataalamu wanasema mwongozo mpya unahitajika katika nyanja hiyo ya utafiti kwasababu wanyama wanaotumiwa kwa utafiti kama huo huenda wakakabiliwa na changamoto itakayozua hofu ikiwa wako nusu hai ama hawajakufa kabisa".
Siku zijazo wanasayansi wanatafakari uwezekano wa kutunza ubongo baada ya mtu kuugua maradhi kama vile kiharusi au mtoto kukumbwa na uhaba wa oxsijeni wakati wa kuzaliwa.

Dkt Andrea Beckel-Mitchener, fkutoka Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya akili nchini Marekani, anasema: "Utafiti kama huu utasaidia kupatikana kwa njia mpya kabisa ya kufanyia ubongo uchunguzi wa kimatibabu.

"Inaweza kuwasaidia watafiti kubuni mbinu ya kuimarisha namna ya kufufua ubongo bada ya kupungukiwa na usambazaji wa damu mwilini ."

Hatahivyo wanasayansi wanasema ni mapema sana kufanya majaribio ya utafiti huu kwa mgonjwa akiumia.

Je uvumbuzi huu utabadili maana ya kifo?

Hapana kwa wakati huu, lakini wataalamu wanasema kuwa wanastahili kujadili ikiwa ubongo wa watu waliokufa unaweza kuwa chanzo cha viungo vya upandikizaji.
Prof Dominic Wilkinson, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, anasema: "Mtu anapobainishwa kuwa ubongo wake ni mfu, uwezekano wa mtu huyo kuponea kifo haupo.

"Inasemekana mtu huyo ameenda kabisa.

"Lakini je kuna uwezekano wa kufufua 'ubongo mfu' au ubongo wa mtu aliyefariki? Hilo likiwezekana basi litatabadili maana ya kifo."

Kwa sasa hilo haliwezekani.


Lakini Utafiti huu unauliza maswali mengi na wakati huo huo kujaribu kupata majibu ya maswali hayo.

Kwa mfano watafiti wanaweza kuweka hai ubongo kwa mda gani?

Je matokeo yangelikua mazuri zaidi laiti hawangesubiri kwa saa nne kabla ya kuanza mchakato wa ufufuzi?

Pia wataalamu hao walitumia dawa ya kudhibiti utendakazi wa ubungo, je wangelipata matokeo sawa laiti hawangelitumia dawa hiyo?
 Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post