MWAKYEMBE AWATAKA WATU WAACHE KUMUULIZIA AZORY GWANDA


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema  watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527