MBUNGE WA KAHAMA MJINI,JUMANNE KISHIMBA : ELIMU YA TANZANIA NI KAMA KIFUNGO CHA MAISHA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 30, 2019

MBUNGE WA KAHAMA MJINI,JUMANNE KISHIMBA : ELIMU YA TANZANIA NI KAMA KIFUNGO CHA MAISHA

  Malunde       Tuesday, April 30, 2019
Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM),  amesema elimu ya Tanzania ni kama kifungo cha maisha.

Akichangia mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, bungeni leo Aprili 30,  Kishimba amesema muda wa kusoma shule Tanzania ni mrefu na unachangia vijana kuzeeka kabla ya kuanza kufanya kazi.

Amesema ni vyema mwaka mmoja mwanafunzi asome madarasa matatu ili kuokoa muda wa kuchukua miaka mingi kabla ya kumaliza shule.

Kishimba ameishauri Serikali iunde tume ya kukusanya maoni kuhusu elimu kwa sababu hali ni mbaya, kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu lakini wapo mtaani kila kona na hawana faida yoyote.

“ Nashauri serikali iunde tume wananchi watoe  maoni ni elimu ipi tuwe nayo.

“ Hivi ni utafiti gani unaosema ubongo wa binadamu kila mwaka usome darasa moja”? tufanye mabadiliko makubwa kwenye sera hii, wenzetu Afrika Kusini nao wanateseka na mfumo kama huu,” amesema Kishimba.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post