MBUNGE CHADEMA AIVAA CCM

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Zainabu Bakari Mussa amedai CCM hawana ubavu ndiyo maana hawawezi kuruhusu tume huru ya uchaguzi.

Zainabu amesema ili CCM wajiamini na kujipima kwa wananchi kama wanakubalika, waweke tume huru ya uchaguzi na kwamba Watanzania watakilaza chama hicho ‘kifo cha mende’.

Akichangia leo Jumatatu Aprili 8, 2019 katika hotuba ya Waziri Mkuu kwa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2019, Zainabu amesema uwanja wa siasa kwa sasa hauko sawa.

Amesema vyama vya siasa vimeminywa na kukosa uhuru wa kufanya siasa zao wakati CCM kunaendelea kufanya siasa, hivyo akaomba katiba mpya aliyosema itajibu yote.

"Kama mnabisha leo hii tuweke makubaliano ili iundwe tume huru ya uchaguzi muone kama 2020 hamtakufa kifo cha mende, narudia mtakufa kifo cha mende kwani Watanzania wa sasa wanaona," amesema Zainabu.

Mbunge huyo amelalamikia suala la kile alichokiita uonevu na ukandamizwaji wanaofanyiwa wapinzani.

Amesema vyama vya upinzani kwa sasa havifanyi siasa kama inavyowapasa wanasiasa, badala yake wanaminywa huku wenzao wa chama tawala wakiruhusiwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post