Picha : WAZIRI KANGI LUGOLA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA POLISI SHINYANGA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga na kushangazwa na kasi ya ujenzi na matumizi kiasi kidogo cha fedha tofauti na jinsi ilivyotarajiwa.


Lugola amejionea hali ya ujenzi huo jana jioni Alhamis Aprili 18,2019 ambapo ujenzi huo unatokana na fedha shilingi milioni 225 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Awali akitoa taarifa,Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula alimweleza Waziri Lugola kuwa ujenzi ulianza Februari 28,2019 na unatarajiwa kumalizika mwezi June mwaka huu na mpaka sasa wamefikia asilimia 75 ya ujenzi.

“Katika ujenzi huu tunashirikiana na Magereza na VETA na tunatumia ‘Local Fundi’,hadi sasa tumetumia shilingi milioni 118, zilizobaki benki ni milioni 107,tunajenga nyumba 10 badala ya 9 zilizopo kwenye mpango”,alieleza Taligula.

“Hizo nyumba 9 zilitakiwa kuwa na vyumba viwili vya kulala,jiko,choo na bafu lakini sisi tunajenga nyumba 10 zenye vyumba vitatu vya kulala ‘kimoja kikiwa ni master room’,jiko,bafu na choo na tunatarajiwa kukamilisha ujenzi mwezi June mwaka huu”,aliongeza Taligula.

Baada ya kukagua ujenzi huo,Waziri Lugola alieleza kushangazwa na kazi nzuri inayofanywa na kamati hiyo ya ujenzi huku akisema kama wangetumia wakandarasi kwenye ujenzi huo huenda zingetumika hata zaidi ya shilingi bilioni moja mpaka sasa.

“Nimeridhishwa na kasi yenu na ubunifu wenu,Mimi kama Waziri nimetembelea miradi mingi,hapa nimekuta vitu vya ziada,nimejifunza mambo mengi, wameongeza idadi ya majengo kutoka lakini pia wamepanua ukubwa wa eneo kwa fedha zile zile shilingi milioni 225 tena wamejenga majengo ya kiwango na ya kisasa ”,alieleza Lugola.

“Nitashauriana na IGP Simon Sirro nimuombe kamati hii iwe ya mfano ,kamati hii itembelee maeneo mengine nchini iwaeleze uzoefu wa kujenga nyumba za kisasa na kwa gharama nafuu kwani hii itatusaidia kujenga nyumba nyingi za makazi ya askari wetu”,alisema Lugola.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na maafisa wa jeshi la polisi alipowasili jana jioni kutembelea na kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula  (kulia) akimweleza Waziri Kangi Lugola kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari eneo la Kambarage Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula akiendelea kuelezea kuhusu ujenzi huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiupongeza uongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi.Aliipongeza kamati ya ujenzi kwa kuwa wabunifu na kujenga majengo ya kisasa kwa gharama nafuu.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akielezea namna jeshi la Magereza na Chuo cha Ufundi Stadi VETA wanavyoshirikana nao katika ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi.
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Muonekano wa jengo la nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao (kushoto) akimwongoza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao (kushoto) akimwongoza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikagua moja ya majengo hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola  akiendelea kukagua majengo hayo.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha nyumba zinazoendelea kujengwa katika eneo la Kambi ya jeshi la polisi Kambarage.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiondoka katika eneo la ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Kambarage mjini Shinyanga jana majira ya saa moja na dakika 45 usiku.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527