JAMAA AMTUPA MTOTO GHOROFANI KISA KUKATALIWA NA WANAWAKE ANAOWAVIZIA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, April 19, 2019

JAMAA AMTUPA MTOTO GHOROFANI KISA KUKATALIWA NA WANAWAKE ANAOWAVIZIA

  Malunde       Friday, April 19, 2019
Mwanamme wa umri wa miaka 24 amekamtawa baada ya kumtupa mvulana wa miaka 5 kutoka orofa ya tatu ya duka moja la bidhaa za jumla huko marekani.

Kwa mujibu wa jamaa huyo kwa jina Emmanuel Aranda, msukumo wa kutekeleza kitendo hicho ulitokana na hasira aliyokuwa nayo baada ya kukataliwa na wanawake kadhaa aliokuwa akiwavizia.

 Kisa hicho kilitokea Ijumaa, Aprili 12 katika duka la mjini Minnesota, wakati wanawake hao walitaja sababu mbali mbali za kumkataa mwanamme huyo.

Emmanuel Aranda alifichua nia yake ya kutaka kuua baada ya kukataliwa na wanawake kadhaa kwenye duka la Minnesota waliotaja sababu mbali mbali.

 Ripoti za shirika la habari la Atlanta zilisema kuwa, mtoto huyo anauguza majeraha mabaya ya kichwani na mifupa kadhaa ambayo imevunjika baada ya kuanguka kutoka urefu wa kina cha futi 40 wa jumba hilo.

 Kwa mujibu wa mamake mwathiriwa, Aranda alimsogelea wakati akiwa ameketi pamoja na wanawake wengine nje ya mkahawa wa Rainforest Cafe. 

Mwanamke huyo aliporajibu kumuuliza iwapo alitaka wampishe, jamaa huyo ambaye hakujibu lolote alimchukua mtoto huyo bila onyo na kumtupa kutoka ghorofa ya tatu walipokuwepo. 

Hata hivyo Aranda alikamatwa papo hapo. 

Mshukiwa alikiri kutekeleza unyama huo na kufichua kuwa siku iliyotangulia alikuja mahali hapo akiwa na nia ya kutaka kumuua mtu bila mafanikio.

 Awali, alifichua kuwa alinuia kumuua mtu mzima lakini kwa kuwa njama yake ilienda kinyume na matarajio yake, aliamua kumuangamiza mtoto huyo.

 "Mshukiwa alidai kwamba, kwa miaka mingi amekuwa akija katika duka hilo kumtafuta mchumba lakini juhudi zake hazikwa zinazaa matunda kwani kila mara alikataliwa. Kila alivyokataliwa, alihisi machungu na kupandwa na mori," mshtakiwa huyo alidai.

 Inasemekana kuwa, Aranda alikuwa amepigwa marufuku dhidi ya kuzuru eneo hilo baada ya kupatikana na hatia ya kuwashambulia watu kadhaa katika matukio mawili tofauti 2015.

 Kwenye kisa kimoja, mtuhumiwa alimrushia glasi ya maji na kisha baadaye ya chai mwanamke aliyedinda kumnunulia kitu alichokuwa akidai katika duka hilo.

 Aidha kutokana na visa hivyo, Aranda aliamuriwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo yupo timamu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post