DEREVA WA GARI DOGO AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI HILO KUGONGANA NA BASI LA MWENDOKASI DAR


Dereva wa gari dogo aina ya Nissan March lenye namba za usajili T968 DNZ amefariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Basi la Mwendokasi eneo la Magomeni Mapipa leo mchana.


Dereva wa gari dogo alikuwa anakata kona kutoka Magomeni kwenda Kariakoo, katika taa za kuongoza magari za Magomeni Mapipa ambazo hazikuwa zinawaka. Ndipo gari dogo likachelewa kupita, na kukutwa katikati ya barabara na Basi la Mwendokasi lililokuwa likielekea Kimara.
 

Baada ya kumpitia, Basi ka Mwendokasi likaichana gari katikati na dereva kufariki pale pale


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post