MWANAMKE AZUA GUMZO BAADA YA KUFUNUA GAUNI NA KUJISAIDIA NDANI YA BENKI



Wateja katika benki moja nchini Afrika Kusini wamepigwa na bumbuazi baada ya kushuhudia maajabu wasiyokuwa wanatarajia. 

Mteja mmoja aliyekuwa mwingi wa hamaki aliamua kuvua nguo na kuamua kukojoa ukumbini mwa benki baada ya kuhisi kuchoshwa na huduma mbovu za benki hiyo.

Katika video iliyosambaa mitandaoni ,mwanamke huyo aliyekuwa mwingi wa hamaki alichutama na kukojoa huku wateja wengine wakimwangalia. 

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alikuwa amesubiri kwa muda wa nusu saa ili wahudumu wa benki hiyo wamfungulie chumba cha kujisaidia lakini walikawia. 

Hata hivyo, baada ya subira yake kufika kikomo aliamua kuchutama na kufanya mambo yake papo hapo alipokuwepo ndani ya benki. 

Wateja wengine aidha, walijawa na sintofahamu kwani walishuhudia tukio ambalo hawakutarajia.

Mwanamke huyo aliyeonekana kutojali watu waliokuwa wamemkodolea macho, aliendelea na biashara yake akiwa ameshikilia rinda lake ambalo alikuwa ameliinua juu wakati akijisaidia.

 Wakati huo wote, la kushangaza hamna yeyote aliyeshughulika kumkaribia wala kumkanya mwanamke huyo dhidi ya kisa hicho. 

Hata hivyo, ni bayana kuwa benki hii itawapoteza wateja iwapo wengi watatilia mkazo kioja walichokishuhudia. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post