IMF: VIKWAZO VYA MAREKANI DHIDI YA IRAN VINAVURUGA UKUAJI WA UCHUMI KATIKA ENEO LA MASHARIKI YA KATI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, April 29, 2019

IMF: VIKWAZO VYA MAREKANI DHIDI YA IRAN VINAVURUGA UKUAJI WA UCHUMI KATIKA ENEO LA MASHARIKI YA KATI

  Malunde       Monday, April 29, 2019

Shirika la Fedha Duniani (IMF) limesema leo kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, kuongezeka kwa machafuko katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na tatizo la bei ya mafuta vinadhoofisha ukuaji wa kiuchumi katika kanda hiyo. 

Mkurugenzi wa IMF wa Idara ya Mashariki ya Kati na ya Asia ya Kati, Jihad Azour, amesema hali hiyo pia inachochea ukosefu wa ajira katika kanda hiyo. 

"Kasi ya polepole ya ukuaji wa uchumi inazua kutengenezwa ajira zinazohitajika ambazo zitawawezesha kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira. Katika miaka mitano ijayo, kanda hiyo inahitaji kuunda nafasi mpya za kazi zaidi ya milioni 25, ili kuimarisha kiwango cha ukosefu wa ajira kinachoshuhudiwa sasa katika kiwango cha juu," amesema Jihad Azour. 

Shirika hilo linatabiri uchumi wa Iran, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika kanda hiyo baada ya Saudi Arabia, utaanguka kwa asilimia 6.0 mwaka huu baada ya kupungua kwa asilimia 3.9 mwaka 2018. 

Uchumi wa Iran umeanza kuporomoka baada ya Marekani kuamua kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo, kufuatia Rais Donald Trump kujitoa katika makubaliano ya silaha za nyuklia ya mwaka 2015.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post