Thursday, April 11, 2019

JAMAA AJIUA BAADA YA KUBAINI ANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

  Malunde       Thursday, April 11, 2019

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 28 kutoka mtaa wa Embakasi jijini Nairobi nchini Kenya amejitoa uhai baada ya kugundua anaishi  na virusi vya HIV.

 Meshack Henry Odhiambo alifariki dunia Jumanne Aprili 9,2019 baada ya kunywa sumu pamoja na kumeza dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs) kupita kiasi. 

Kulingana na stakabadhi zake kutoka hospitali ya Mbagathi, Odhiambo aliamua kujitoa uhai dakika chache tu baada ya kutembelea kituo cha afya ambapo alikuwa amekwenda kujua hali yake ya kiafya. 

 "Alikuwa na afya nzuri kabisa kando na kukohoa mfululizo kwa zaidi ya majuma mawili yaliopita, hakuna aliyetarajia kwamba angekuwa na virusi hivyo," Mmoja wa jamaa wake alisema. 

" Odhiambo alienda hospitalini na akafanyiwa vipimo vya kifua kikuu na vya Ukimwi, kwa bahati mbaya , alipatikana na virusi vya HIV, alirejea nyumbani akiwa mwingi wa mawazo na hivyo ndivyo alijiua," Rafiki yake alisema. 

Aidha, jirani wake alishangazwa na kifo chake na kudai kuwa marehemu hakuonekana kuwa mtu aliyependa raha ila alikuwa akimuona na mpenzi mmoja tu. 

Chanzo - Tuko
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post