HARAMBEE YA JOKATE MWEGELO YAKUSANYA MILIONI 915


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo, ameeleza kuwa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.

Uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na Jocate kwa kushirikiana na viongozi wengine.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mwegelo amesema baada ya kuzindua harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi huo wameamua  kutoa mrejesho kwa Watanzania wa nini ambacho kimepatikana.


"Tumefanikiwa kupata Sh 915,174,000 kati ya Sh 1.38 bilioni ambazo zilikuwa ndio lengo letu katika harambee iliyofanyika kwetu ni mafanikio makubwa yanayowezesha kuanza ujenzi" amesema Jokate na kuongeza kuwa  fedha hizo zinajumuisha ahadi,vifaa vilivyotolewa pamoja na fedha taslimu Sh 80,641,000 .

"Ziko ahadi nyingi zilizotolewa ikiwamo madarasa sita ambayo ni sawa na Sh 120 milioni, mabweni mamwili sawa na Sh160 milioni, maabara, mifuko 1,890 ya simenti, mbao pamoja na mabati," amesema

Amesema anawashukuru wananchi wa Tanzania na wadau wa maendeleo waliojetokeza kuchangia kampeni hiyo ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu, ingawa kwa siku za usoni watajenga na ya watoto wa kiume kwani kupanga ni kuchagua.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527