FISI WAZUA GUMZO NA KUWA TISHIO KAHAMA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 30, 2019

FISI WAZUA GUMZO NA KUWA TISHIO KAHAMA

  Malunde       Tuesday, April 30, 2019
Kundi kubwa la  wanyama aina ya fisi limewajeruhi watu  watano  sehemu mbalimbali za miili yao katika  kata za  Nyandekwa na Kilago halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wakati wakijaribu kupambana na fisi hao waliovamia makazi ya watu.

Diwani wa Kata ya Kilago PETER EMANUEL amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  April 28,2019  ambapo  majeruhi watatu hali zao bado hazijaimarika na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mji wa Kahama  na kwamba wananchi katika maeneo hayo amejawa na hali ya wasiwasi.

Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama, baadhi ya  majeruhi wameiomba serikali  kuwadhibiti fisi hao kwani wanaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi na kwamba wamekuwa wakipambana nao mara kwa mara.

Afisa maliasiri  halmashauri ya mji wa Kahama, THOMAS MANUMBU amesema  tatizo la Fisi kuvamia makazi ya watu   bado lipo kwa wingi katika kata za pembezoni tangu mwezi wa pili mwaka huu  huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati serikali inaendelea kupambana na  fisi hao.

Kwa upande wake Mhifadhi wa wanyanama Tanzania  (TAWA) wilaya ya Kahama, MAPANYA KARUTO  amewataka wananchi kutumia toshi nyakati za usiku na kwamba waondokane na imani za kishirikina  dhidi ya uwepo wa fisi hao.

 Credit - Kahama FmUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post