Picha : FISI AVAMIA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KISHAPU,AUA MBUZI NA KONDOO 16

Katika hali isiyokuwa ya kawaida fisi amevamia nyumbani kwa Diwani wa kata ya Lagana ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,Boniface Butondo kisha kuua mbuzi na kondoo 16. 

Butondo ameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2019 majira ya 10 alfajiri katika kijiji cha Lagana ambapo fisi huyo ameshambulia watoto wa mbuzi na kondoo katika nyumba ya mifugo hao wapatao 16. 

“Ilikuwa majira ya saa 10 alfajiri ndipo fisi huyo alipoingia katika nyumba hiyo na baada ya kusikia makelele ya mbuzi na kondoo hao wadogo wanafamilia wakaamua na kuita majirani wazingira nyumba kwa marungu, mikuki,mawe na pia kufanya kazi ya kufumua paa juu ,wakafanikiwa kumuua majira ya saa 1 na tayari alikuwa ameshakula watatu na kuua wengine 13 na kubakiza wanne ”,ameeleza Butondo. 

“Mimi ni mfugaji wa mbuzi na kondoo,hao watoto wa mbuzi na kondoo nimejengea nyumba yao,mbuzi na kondoo wakubwa nao banda lao,kwa kweli tukio hili limenisikitisha sana na limetokea wakati mimi sipo nyumbani”,ameongeza Butondo.

Na Kadama Malunde - Malunde1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post