WAZIRI MBARAWA AAGIZA MKANDARASI WA MAJI AKAMATWE


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, ameagiza kukamatwa ndani kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ukandarasi PET CO Operation, inayojenga mradi wa chujio la Maswa katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Tryphone Elias, kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.


Mradi huo unaogharimu kiasi cha Sh bilioni 3.5,  ulitakiwa kujengwa kwa muda wa miezi minane lakini umetimiza miaka minne tangu mwaka 2015 bila ya kukamilika ujezi wake.

Jana usiku Waziri huyo alifanya ziara ya ghafla kukagua ujenzi unavyoendelea kabla ya kutoa maagizo hayo Waziri huyo alisema kuwa mkadarasi huyo amepewa miradi 15 kwenye maeneo mbalimbali nchini, ambayo yote imeshindwa kukamilika kwa wakati.

“Pale Wizarani ulitumia njia za rushwa ukapewa hii miradi, haiwezekani miradi yote 15 mtu mmoja na yote imemshinda, hakuna mradi ambao umekamilisha ujenzi wake, umeendelea kukatili wakazi wa Mji wa Maswa kutumia maji yenye tope,” amesema Waziri Mbarawa.

Baada ya kusema hayo, aliwataka Kamanda wa Polisi Wilaya ya Maswa na Mkuu wa Wilaya kusimamia Mkandarasi huyu akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa mbili na muda huo ukiisha aandike maelezo ndani ya siku 11 awe amekamilisha akishindwa kuandika hayo maelezo vizuri asitoke.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post