TAASISI YA APHFTA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI 2019


Kila mwaka Aprili 25 huwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambapo kwa mwaka huu 2019, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya imekuja na mkakati wa “Zero Malaria” unaolenga kutokomeza Malaria hadi kufikia mwaka 2030. Kitaifa maadhimisho ya siku ya Malaria 2019 yamefanyika mkoani Lindi yakiwa na kaulimbiu isemayo “ZeroMalaria inaanza na mimi” huku mikoa mingine nayo ikipata fursa ya kuandaa maadhimisho yake.

Katika Mkoa wa Geita, Chama cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA) kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa afya, kimeandaa maadhimisho haya kimkoa katika shule ya msingi Mkapa iliyopo Mji Mdogo Katoro ambapo huduma mbalimbali ikiwemo upimaji wa Malari bure kutolewa kwa wananchi.

Chama cha APHFTA kimekuwa ikitekeleza mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita kuanzia mwezi Januari mwaka 2017 unaotarajiwa kufikia tamati mwezi Disemba mwaka huu ambapo mradi huo na mikakati mingine, umesaidia kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi asilimia 17.3 mwaka 2017/18.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita kwenye Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 mkoani humo yaliyofanyika kwenye viunga vya Shule ya Msingi Mkapa iliyopo katika Mji Mdogo wa Katoro.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita kwenye Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 mkoani humo.
Mratibu wa Udhibiti Malaria Mkoa Geita, Dkt. Moses Simon akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Tanzania inazidi kupiga hatua kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao vimelea vyake huenezwa na mbu jike aina ya “Anopheles” ikielezwa kwamba maambukizi
yameshuka kwa asilimia 50. Malaria ni hatari kwa sababu mtu mmoja hupoteza maisha duniani kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi (katikati) akiwa ameshika bango la "Ziro Malaria, Inaanza na Mimi" ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mkakati wa Serikali kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030.
Wakati chanjo mpya ya Malaria inayotambulishwa na Shirika la Duniani (WHO) ikitarajiwakufanyiwa majaribio katika nchi za Kenya, Malawi na Ghana, Serikali ya Tanzania imetenga shilingi Bilioni 12.5 ili kutekeleza program mbalimbali za kupambana
na Malaria hususani katika wilaya 10 nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi.
Wilaya zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria Tanzania ni Kakonko yenye asilia 30.8, Kasulu asilimia 27.6, Kibondo asilimia 25.8, Uvinza asilimia 25.4, Kigoma asilimia 25.1, Buhigwe asilimia 24, Geita asilimia 22.4, Nanyamba asilimia 19.5, Muleba asilimia 19.4 na Mtwara asilimia 19.1.
Juhudi za kupambana na Malaria ni pamoja na kutokomeza mazalia ya mbu, kugawa bure na kuhamasisha matumizi ya vyandarua vyenye dawa, kunyunyizia dawa za kuua mbu majumbani, kutoa elimu kwa wananchi ili kuweka mazingira yao safi, kuwahi hospitalini wanapohisi viashiria vya Malaria ikiwemo joto kali na kutapika.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 kwa Mkoa Geita yaliyofanyika katika Mji Mdogo wa Katoro.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akikagua zoezi la upimaji Malaria kwenye maadhimisho hayo.
Tanzania inazidi kupiga hatua kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao vimelea vyake huenezwa na mbu jike aina ya “Anopheles” ikielezwa kwamba maambukizi
yameshuka kwa asilimia 50. Malaria ni hatari kwa sababu mtu mmoja hupoteza maisha duniani kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo.
Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa na asilimia 14.4 ya maambukizi ya Malaria ambapo juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zimesaidia kiwango hicho kitaifa kupungua hadi asilimia 7.3 mwaka huu. Hata hivyo juhudi zaidi zinahitajika
kwani kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO),Tanzania ina asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na Malaria.
Idadi kubwa ya wananchi ilijitokeza kupima Malaria bure.
Mmoja wa wakati wa Katoro mkoani Geita (katikati) akiwa kwenye bango la "Ziro Malaria, Inaanza na Mimi" ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mkakati huo wa kutokomeza Malaria Tanzania ifikapo mwaka 2030. Kushoto ni Mratibu wa Udhibiti Malaria Mkoa Geita, Dkt. Moses Simon na kulia ni Bigeso Makenge ambaye ni Mratibu wa Mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita unaotekelezwa na APHFTA kuanzia Januari 2017 hadi Disemba 2019.
Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa na asilimia 14.4 ya maambukizi ya Malaria ambapo juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zimesaidia kiwango hicho kitaifa
kupungua hadi asilimia 7.3 mwaka huu. Hata hivyo juhudi zaidi zinahitajika kwani kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania ina asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na Malaria.
Aidha matokeo ya utafiti wa viashiria vya Malaria Tanzania mwaka 2017 yanaonyesha Mkoa wa Kigoma unaoongoza kwa kiwango kikubwa cha ugonjwa huo ukiwa na asilimia 24 ukifuatiwa na Geita asilimia 17, Kagera na Mtwara asilimia 15, Tabora,
Ruvuma na Lindi asilimia 12 hii ikiwa ni mikoa yenye kiwango cha juu cha maambukizi.
Taasisi ya APHFTA iligawa vipeperushi vyenye elimu kuhusu Malaria kwenye maadhimisho.
Mikoa inayofuatia ni Mara yenye asilimia 11, Morogoro
asilimia 10, Mwanza asilimia nane, Katavi asilimia saba, Simiyu na Shinyanga asilimia sita, Pwani asilimia tano, Mbeya asilimia nne, Tanga asilimia tatu, Singida, Rukwa na Iringia asilimia mbili, Dar es salaam, Dodoma na Mjini Magharibi Zanzibar asilimia moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post