KILICHOMFANYA ZAHERA ABAKI DAR CHAJULIKANA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 17, 2019

KILICHOMFANYA ZAHERA ABAKI DAR CHAJULIKANA

  Malunde       Sunday, March 17, 2019

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera

Tetesi zinaeleza kuwa kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ataondoka hii leo na ndege moja na wachezaji wa AS Vita Club ili kuwahi katika majukumu ya timu ya taifa ya Congo ambayo tayari iko kambini tangu wiki iliyopita.

Zahera alihitajika kujiunga katika kambi hiyo Machi 13 lakini alibaki nchini kwa maagizo ya bosi wake, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya DRC, Florent Ibenge ambaye pia ni kocha mkuu wa AS Vita. 

Mwinyi Zahera alibaki nchini kuufuatilia mchezo wa AS Vita na Simba SC kwa kuwa AS Vita ina zaidi ya wachezaji watano wanaounda kikosi cha kwanza cha DR Congo.

Kabla ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kati ya Simba na AS vita Club, jana Machi 16, mashabiki wa Simba pamoja na Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara walionekana kuchukizwa na kitendo walichokiita cha usaliti ambacho kocha huyo anafanya, kwa kuahirisha safari ya kwenda Congo na kuamua kubaki na AS Vita hapa Dar es salaam.

Hali hiyo ilileta sintofahamu kwa mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakimhofu Mwinyi Zahera kuwa kutokana na kuwafahamu vizuri Simba, angeweza kumpa bosi wake, Florent Ibenge mbinu mbalimbali za Simba.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post