WAZIRI MKUU KUFUNGUA SOKO LA DHAHABU GEITA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua soko la dhahabu mkoani Geita, Alhamisi Machi 14, 2019 mwaka huu likiwa ni soko la kwanza nchini katika madini ya dhahabu na la tatu kwa ukubwa barani Afrika.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Machi 11, 2019 amesema mkoa huo unaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu kwa zaidi ya asilimia 40 ya dhahabu yote inayozalishwa nchini.

Amesema soko kuu la dhahabu litakalokuwa eneo la soko kuu mjini hapa litakuwa na wadau wote walio kwenye mnyororo wa biashara ya madini wakiwemo wanunuzi, wauzaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Madini, benki na mamlaka ya serikali za mitaa.

Amesema kuwepo kwa wadau wote eneo moja kutaondoa urasimu na kurahisisha kufanyika biashara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post