KAULI YA JOSHUA NASSARI BAADA YA KUVULIWA UBUNGE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 15, 2019

KAULI YA JOSHUA NASSARI BAADA YA KUVULIWA UBUNGE

  Malunde       Friday, March 15, 2019

Joshua Nassari.
Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amedai kuwa kitendo cha kuvuliwa ubunge ni uonevu dhidi yake, na kusisitiza kuwa fikra hizo zipuuzwe.

Nassari ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Spika Job Ndugai alipomwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC,) Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu kuhusu jimbo hilo la Arumeru Mashariki kuwa wazi baada ya mbunge wake kupoteza sifa.

Nassari amesema kuwa kesho atazungumza na vyombo vya habari kwa undani, na kuahidi kuitafuta haki popote na kwamba alikuwa kimya kwa kuiheshimu sheria.

"Watanzania wenzangu na Watu wangu wa Arumeru. Tumefanyiwa dhuluma na uonevu. Nitazungumza kesho na vyombo vya habari kwa undani kuhusu jambo hili. Tutaitafuta haki popote. Katika hatua ya sasa, puuzeni fikra hasi zinazoenezwa na maadui zetu dhidi yangu, hata hivyo niliheshimu sheria na vielelezo vipo", ameandika Nassari.

Mbunge huyo amevuliwa ubunge akiwa anatekeleza majukumu ya kibunge kwa sababu alikuwa katika ziara ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyokuwa Chuo cha Mwika, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post