Wednesday, March 13, 2019

MWARABU ALIYEKABIDHIWA SIMBA ANATISHA

  Malunde       Wednesday, March 13, 2019


Refarii wa Morocco
Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Simba SC dhidi ya AS Vita, wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kutokana na mwamuzi wa mchezo huo Noureddine El Jaafari kusifika kwa kumwaga kadi na kutoa penati.

Noureddine El Jaafari raia wa Morocco, ameteuliwa na CAF kuchezesha mchezo huo wa Jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo refa huyo ni mkali awapo kwenye majukumu yake.

Akiwa tayari ameshachezesha mechi kadhaa za hatua ya makundi msimu huu, Noureddine El Jaafari ameshatoa jumla ya kadi 18. Kati ya hizo kadi za njano ni 16 na kadi nyekundu ni 2.


Moja ya mechi ambayo Noureddine El Jaafari alichezesha na kutoa kadi nyingi ni ile ya kundi C kati ya CS Constantine dhidi ya TP Mazembe ambao ulimalizika kwa Mazembe kupoteza kwa mabao 3-0 huku yeye akitoa kadci 4 za njano ikiwa ni mbili kwa kila timu.

Wachezaji wa Simba ambao wamekuwa wakipata kadi za njano ni pamoja na Jonas Mkude, Juuko Murshid, Cletous Chama, Paul Bukaba pamoja na Emmanuel Okwi, hivyo wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi katika mchezo huo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post