KUTANA NA SAMAKI HUYU WA PEKEE ALIYESOMBWA NA MAJI

Samaki ambaye ni nadra kupatikana anayeaminiwa kuwa anaishi katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia amesombwa hadi kwenye ufukwe wa Santa Barbara, California.

Kupatikana kwa samaki huyo mwenye futi saba sawa na (2.1m) kumewashangaza wanasayansi ambao wanajiuliza ni kwa vipi aliweza kusafiri kutoka kwenye makazi yake ya majini.

Mwanafunzi aliyeko mazoezini katika Chuo Kikuu cha California alimuona samaki huyo katika kituo cha hifadhi ya mali asili cha Coal Oil Point.

Iliwachukua watafiti siku kadhaa kumtambua kiumbe huyo ambacho kiligundulika kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014.

Picha za samaki huyo mwenye umbo kubwa zilionekana kwenye ukurasa wa kituo cha Coal Oil point na wataalam kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wakakusanyika kusaidia kumtambua kiumbe huyo wa aina yake.

Myama huyo ilipewa jijna la "hoodwinker" baada ya uvumbuzi wake kuwatatiza watafiti kwa miaka mingi.

Marianne Nyegaard, ambaye ni mwanasayansi wa viumbe wa majini ambaye alimgundua na kumuita jina samaki huyo, aliiambia televisheni ya Marekani CNN kwamba "karibu nianguke kutoka kwenye kiti changu " nilipoiona picha ya samaki huyo''

"Wakati nilipopata picha halisi sikuwa na wasi wasi ," alisema. "Ni shauku iliyomfanya samaki huyo avuke uzio wa Ikweta."

Hoodwinker ni samaki mkubwa sana na ambaye anateleza kuliko samaki wengine wa kizazi cha samaki wa jua (sunfish) , akiwa na uzito wa tani mbilili sawa na kilogramu 2000.

Samani wa aina yake wanasemekana kupenda zaidi maji yenye viwango vya joto vya juu, kama vile kwneye maeneo ya mwambao wa Chile au New Zealand.

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527