POLISI AMUUA MKEWE KWA RISASI AKIMTUHUMU KUZAA NA MCHEPUKO


Wimbi  la simanzi limewagubika wenyeji wa kijiji cha Kaunda eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega nchini Kenya baada ya afisa wa polisi wa utawala (AP) Patrick Nyapara kumuua mkewe Christine Maonga (28) kwa kumpiga risasi kichwani.


Kwa mujibu wa majirani, wawili hao wamekuwa wakizozana kuhusu mwanao ambaye jamaa alidai sio wake
 kwamba Mwanamke huyo ambaye alikuwa akihudumu kama mwalimu katika shule ya upili ya Navakholo alichepuka nje ya ndoa yao.

 Christine Maonga  anadaiwa kuuawa na mumewe Patrick Nyapara ambaye ni afisa wa polisi wa utawala katika kituo cha Navakholo, kaunti ya Kakamega  kwa kupigwa risasi mara tatu kichwani baada kuzozana kwa muda mrefu.

Nyapara alidai kuwa mkewe alipata ujauzito nje ya ndoa na kumsingizia kuwa yeye ndiye baba wa mtoto huyo baada ya kujifungua.

 Kulingana na ripoti zilizofikia TUKO.co.ke, inadaiwa kuwa ndoa ya wawili hao imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba pindi tu mwanamke huyo alipojifungua mtoto wao wa kwanza.

Mara kwa mara wamekuwa wakizozana jambo ambalo limekuwa likimlazimu mwanamke huyo kutorokea kwao. 

Tulishangaa kumuona mwanamme wa boma hili akija nyumbani huku amevalia magwanda rasmi ya polisi jambo ambalo hatujawai kushuhudia" mmoja wa mashuhuda alisema.

 "Mzee ni mtu mpole na mwenye maneno machache, alipoingia nyumbani walianza kuzozana kwa sauti ya juu na mkewe. Tulijaribu kuwatuliza lakini juhudi zetu hazikufua dafu . Tulimnasua mtoto huyo kutoka kwa nyumba hiyo tukawaacha wakizozana na mkewe kwasababu ilikuwa ni kawaida yao kugombana, baada ya dakika chache tukasikia milio ya risasi tuliporudi kuangalia tulipata christine ameuawa" ,aliongezea mdokezi. 

 Inaelezwa kuwa mwanamme huyo amekuwa akimtishia mkewe hata katika mitandao ya kijamii. 

Afisa huyo alitoweka baada ya kutenda kitendo hicho huku mwili wa marehemu ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini kakamega. Marehemu alikuwa mwalimu katika shule ya Upili ya Navakholo. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post