Picha : POLISI SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA POLISI NA FAMILIA, WAMPONGEZA MAGUFULI UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARIJeshi la Polisi mkoani Shinyanga limeadhimisha siku ya polisi na familia (Police Family Day 2019), kwa kuonesha jinsi linavyofanya kazi ya kulinda amani ya nchi na kusimamia sheria za usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya kuaga mwaka 2018 na kuukaribisha rasmi mwaka 2019.


 pamoja na kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa nyumba Tisa za askari Polisi.

Sherehe hizo zimefanyika leo Machi 22,2019 kwenye Viwanja vya Polisi Kambarage Mjini Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa amani, ambao wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulinzi wa amani.

Akizungumza kwenye sherehe hizo Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amelipongeza Jeshi  la Polisi kwa kazi nzuri linazozifanya kwa kuhakikisha amani ya  nchi inaendelea kutawala.

Alisema Jeshi la polisi muhimu sana katika nchi ambayo inataka kukua kimaendeleo na kuwataka waendelee kujituma kufanya kazi kwa bidii na weledi, kwa kuilinda amani ya nchi ili wananchi waendelee kufanya shughuli za kiuchumi bila ya kuwa na wasiwasi.

“Nalipongeza sana Jeshi letu la Polisi mkoani Shinyanga kwa kuendelea kulinda amani ya nchi, ambapo mkoani kwetu hapa hali ni shwari kabisa na hata kwenye wilaya zake hakuna matukio ya kutisha, hivyo endeeleni kufanya doria na misako mikali kabisa na kuwa dhibiti wahalifu mapema kabla ya kuleta madhara,” alisema Mboneko.

“Pia nawasihi muendelee kuwa na nidhamu kazini na kuacha tabia ya kuomba rushwa bali mfanye kazi zenu kwa kufuata maadili, kitendo ambacho mtafanikiwa kukomesha kabisa matukio ya uhalifu pamoja na kumaliza ajali za barabarani,” aliongeza.


Katika hatua nyingine alilitaka Jeshi hilo kuhakikisha linajipanga vyema kulinda amani na utulivu kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu, na kusiwepo kabisa na uvunjifu wowote wa amani, ili wananchi waweze kuwachagua viongozi ambao wanawataka.

Naye Kamanada wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, LIsema Jeshi hilo limejipanga vizuri katika kuhakikisha linatokomeza matukio ya uhalifu mkoani humo, huku likiwataka wananchi kuendelea kushirikiana nalo kwa kutoa taarifa mapema za watu ambao wanataka kuvunja amani ili waweze kutiwa nguvuni kabla ya kuleta madhara.

Alisema kwa takwimu za mwaka Jana (2018) wameweza kupunguza makosa ya uhalifu 706 ambayo yalikuwa makosa 13,621, ambapo mwaka Juzi (2017) kulikuwa na makosa ya uhalifu 14,327, na kubainisha kuwa kwa mwaka huu (2019) wamejipanga vyema kupunguza kwa kiasi kikubwa makosa hayo ya uharifu.

Pia alimpongeza Rais John Magufuli kwa kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 200.25 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba tisa za askari Polisi Shinyanga Mjini, hali ambayo itapunguza tatizo la uhaba wa nyumba za polisi na kuishi kwenye makazi bora.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto)  kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Zainab Telack, akiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, kwa ajili ya kufungua sherehe  ya "Police Family" kwa kukagua Gwaride pamoja na kutoa zawadi kwa askari waliofanya vizuri mwaka uliopita (2018). - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Askari wakielekea kujipanga kwenye mstari tayari wa ukaguzi wa Gwaride.
Askari wakijiweka sawa tayari kwa ukaguzi wa Gwaride.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua Gwaride.

Ukaguzi wa Gwaride ukiendelea.

Ukaguzi wa Gwaride ukiendelea kabla ya kuanza maadhimisho ya Police Family Day.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akitoa zawadi kwa askari waliofanya vizuri mwaka (2018) katika vitengo mbalimbali.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea kwa askari waliofanya vizuri mwaka uliopita 2018.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea kwa askari waliofanya vizuri mwaka uliopita 2018.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea kwa askari waliofanya vizuri mwaka uliopita 2018.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.

Askari Polisi waliopokea zawadi kwa kufanya vizuri mwaka uliopita 2018 wakiwa kwenye mstari wa pamoja.

Askari Polisi wakitoa heshima kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko mara baada ya kumaliza kukagua Gwaride na kutoa vyeti kwa askari waliofanya vizuri mwaka uliopita.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na zoezi la ugawaji vyeti vya shukrani kwa wadua ambao wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi, wakiwamo Gilitu Company, Jambo, Ghaki, Ahamu, CRDB, Kahama Oil Mil, Save the children, Mgodi wa Buzwagi, Mwadui, pamoja na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Zoezi la utoaji vyeti vya shukrani kwa wadau wa Jeshi la Polisi likiendelea.

Zoezi la utoaji vyeti vya shukrani kwa wadau wa Jeshi la Polisi likiendelea.

Zoezi la utoaji vyeti vya shukrani kwa wadau wa Jeshi la Polisi likiendelea.

Zoezi la utoaji vyeti vya shukrani kwa wadau wa Jeshi la Polisi likiendelea.

Zoezi la utoaji vyeti vya shukrani kwa wadau wa Jeshi la Polisi likiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Makamu mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley, ambaye pia ni Mwandishi wa habari Star Tv.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao akimkabidhi zawadi ya heshima mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akionyesha zawadi ya heshima ambayo amepewa na Jeshi la Polisi.

Askofu Raphael Machimu wa kanisa la (EAGT Ushirika wa Shinyanga) akitoa maombi kabla ya Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kuanza kutoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya Police Family Day.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisoma hotuba yake kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Zainab Telack amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda amani ya nchi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, akisoma hotuba yake amebainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kutawala kwa kufanya Doria na Misako mbalimbali ya kuwatia nguvu mapema wahalifu kabla hawajaleta madhara.

Askari wakisiliza kwa makini nasaha za viongozi wao katika kuendelea kulitumikia taifa hili, ili amani na utulivu viendelee kutawala.

Askari wakiendelea kusikiliza kwa makini nasaha za viongozi wao.

Baadhi ya familia za Jeshi la Polisi wakiwa kwenye maadhimisho ya Police Family Day.

Askari Polisi wakiwa na familia zao.

Jeshi la Zimamoto nalo likiwa kwenye maadhimisho ya Police Family Day.

Askari Magereza wakiwa kwenye maadhimisho ya Police Family Day.

Wadau wa Jeshi la Polisi pamoja na viongozi wa dini wakiwa kwenye maadhimisho ya Police Family Day.

Wadau wa Jeshi la Polisi wakiwa kwenye sherehe za Police Family Day.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakionyesha namna wanavyopambana na wahalifu ambao nao hutumia salaha za moto.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakionyesha namna wanavyopambana na wahalifu ambao nao hutumia salaha za moto.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani nao wakitoa elimu kwa wananchi namna ya kuvitumia vivuko hasa kwa kuwavusha wanafunzi ili kuepukana na ajali za barabarani.

Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi nalo likionyesha Jinsi gani linavyoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia.

Vijana wakitoa burudani ya kuruka sarakasi kwenye maadhimisho hayo.

Mburudishaji kutoka kundi la Shinyanga Art nae akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.

Mofisa wa Polisi wakipiga picha ya Pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, mara baada ya kumaliza maadhimisho hayo ya Police Family Day pamoja na kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha 2019.

Mara baada ya kuhitimisha maadhimisho hayo ya Police Family Day Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha ujenzi wa nyumba tisa za askari Polisi Shinyanga Mjini unavyoendelea. Fedha za ujenzi zimetolewa na Rais John Magufuli Shilingi Milioni 200.25 ili kuwaondolea upungufu wa makazi.

Wandishi wa habari Mkoani Shinyanga nao wakihitimisha kuchukua matukio  kwenye madhimisho hayo ya siku ya Polisi Family, wa kwanza kushoto ni Frank Mshana wa ITV, akifuatiwa na Shabani Alley wa Star Tv na  kulia ni Suleiman Abeid mwandishi wa gazeti la Majira na TV Imani.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post