ANUSURIKA KUFA KWA KUKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI...MWANAFUNZI WA KIKE ADAKWA


Picha haihusiani na habari hapa chini

Mtu mmoja mkazi wa Marangu mkoani Kilimanjaro amenusirika kufa baada ya vijana kumkamata na kuzikatia chini sehemu zake za siri.


Mtu huyo mwenye umri wa miaka 53 amesema, tukio hilo lilimtokea juzi wakati akitoka katika shughuli zake za kila siku ndipo alikutana na vijana wawili ambao walianza kumpiga.

"Nilitoka kazini muda wa saa tatu usiku nikiwa napandisha nyumbani, nikakutana na vijana, mmoja akanipiga na chuma mgongoni nikaanguka chini, mwingine akachomoa sime akachana suruali nliyokuwa nimevaa na kunikata sehemu zangu,"alisema.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issah alisema, tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Marera lole Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani humo.

Alisema kuwa, mtu huyo alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kwa kukatwa sehemu za siri akiwa maeneo ya karibu na nyumbani kwake.

Alisema kuwa , waliomjeruhi ni Inocent Rubi mwenye umri wa miaka 18 na mwingine anayeitwa Gift Olmekei ambaye ni mtoto wa kike ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiri na kusema wote wameshikiliwa na Jeshi la Polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Aliendelea kusema kuwa, mara baada upelelezi utakapokamilika shauri hilo litapelekwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili waweze kujua mtu huyo alitoka wapi na watoto wadogo ambao ni wanafunzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527