WAZIRI MPINA ATANGAZA KUUNDWA KANDA KUU MPYA YA ULINZI WA RASILIMALI BAHARI YA HINDI

Wananchi wa Kilwa Kivinje wakishangilia na kusalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb), mwenye koti la bluu mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara. Picha na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb),mwenye miwani akiwasili katika eneo la Kilwa Kivinje kuongea na wavuvi hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngubiagai na kushoto ni diwani Ali Mohamed Yusufu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb) akiwahutubia wananchi wa Somanga Kilwa.


Na John Mapepele, Kilwa

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametangaza kuundwa kanda kuu mpya ya ulinzi wa rasilimali katika Bahari ya Hindi ili kukabiliana na uvuvi haramu ulioshamiri kwa muda mrefu. 

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano ina nia thabiti ya kulinda rasilimali hizo ili ziweze kulinufaisha Taifa.

Mpina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati akizungumza na wavuvi wilayani Kilwa mkoani Lindi kuhusiana na juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kulinda rasilimali hizo na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya maombi ya wavuvi ikiwemo kuomba kuruhusiwa kutumia majenereta na taa za sola kaatika shughuli zao za uvuvi wawapo baharini baada ya Sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003 kukataza za vifaa hivyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wavuvi katika maeneo ya Kivinje na Somanga wilayani Kilwa Waziri Mpina alisema Serikali ya awamu ya tano haina nia kumuonea mwananchi yeyote bali kinachofanyika ni kulinda rasilimalli hizo kwa mujibu wa sheria ili ziwe enedelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mpina alisema katika kuwasikiliza wavuvi nchini Serikali imeamua kufumua Sheria ya Uvuvi na kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa maeneo ambayo yanakwaza shughuli za uvuvi ikiwemo kufuta vipengele vilivyokuwa vinalalamikiwa kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mpina alikubali ombi la wavuvi nchini kurusiwa kutumia taa za sola na majenereta huku akitaka wavuvi ha kutokamatwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni hadi hapo kanuni mpya zitakapotoa Julai mwaka huu.

Pia aliwaomba wavuvi kuwa na subira kuhusiana na ombi la kutaka kuruhusiwa kutumia nyavu za chini ya milimita nane kwani kwani sheria iliyopo ya uvuvi ya mwaka 2003 na Kanuni yake ya mwaka wa 2009 imeweka masharti kuzuia matumizi ya nyavu hizo kwenye ukanda wa bahari hivyo kuwataka kuwa watulivu na kusubiri sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa christopher Ngubiagai alimshukuru Waziri Mpina kwa kufika kuzungumza na wananchi hao kwani ametoa ufafanuzi utakaoondoa sintofahamu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wavuvi wa wilaya hiyo huku akiwaomba kuunga mkono juhudi za serikali za kulinda rasilimali za uvuvi.

Mmoja wa wavuvi wa Somanga Mohamedi Kimbwembe aliomba radhi Serikali ya awamu tano kutokana na wavuvi wengi kujihusisha na uvuvi haramu na kuua mazalia ya samaki na kwamba wengi walifanya hivyo baada ya serikali zilizopita kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya waalifu hao.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Lindi Hamida Abdalha alimshukuru Waziri Mpina kwa kuruhusu matumizi ya jenereta na taa za mwanga wa jua pamoja na kuruhusu wavuvi kutumia leseni moja mambo ambayo yalikuwa yakiwaumiza wavuvi wa Lindi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527