KIBONDE KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI

Mtangazaji maarufu wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde, anatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, sehemu ambayo alizikwa mke wake, Sarah, aliyefariki dunia Julai, mwaka jana.

Kibonde alifariki dunia juzi jijini Mwanza kwa shinikizo la damu wakati jitihada za kumhamishia Hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando kutoka Hospitali ya Uhuru zikifanyika.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, mtangazaji huyo ataagwa leo nyumbani kwa wazazi wake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na baadaye saa 10:00 jioni atazikwa makaburi ya Kinondoni.

Kibonde alianza kujisikia vibaya kabla ya kuzikwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa CMG, Ruge Mutahaba, Bukoba mkoani Kagera na kupelekwa Hospitali ya rufani ya Mkoa wa Kagera ya Bukoba na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Uhuru. Wakati akipelekewa Bugando, ndipo umauti ulipomkuta alfajiri ya kuamkia juzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post