MAMIA YA WANACHAMA CUF KUTOKA KATA 27 NA MATAWI 96 TANGA WAHAMIA ACT-WAZALENDO KUUNGANA NA MAALIM SEIF | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 19, 2019

MAMIA YA WANACHAMA CUF KUTOKA KATA 27 NA MATAWI 96 TANGA WAHAMIA ACT-WAZALENDO KUUNGANA NA MAALIM SEIF

  Malunde       Tuesday, March 19, 2019


Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) jijini Tanga, kutoka kata 27 na matawi 96, wamemfuata aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif, ACT- Wazalendo na kukabidhiwa kadi za uanachama.

Wakati wanachama hao wakifanya uamuzi huo, leo Jumanne Machi 19, jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amekabidhiwa rasmi kadi namba moja ya ACT-Wazalendo iliyolipiwa ada ya miaka 10.

Wanachama hao pia, wamechoma kadi zao za zamani na bendera za CUF, kuashiria kwamba wamejivua uanachama wa chama hicho na sasa wao ni rasmi wanachama wa ACT-Wazalendo.

Wamesema wameamua kumuunga mkono maalimu Seif kujiunga ACT Wazalendo kwani ndio chama makini kinachoweza kuwafikisha kwenye azma yao ya kuiondoa CCM madarakani.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post