MWALIMU MKUU AFARIKI DUNIA GHAFLA NYUMBANI KWA MGANGA WA JADI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 13, 2019

MWALIMU MKUU AFARIKI DUNIA GHAFLA NYUMBANI KWA MGANGA WA JADI

  Malunde       Wednesday, March 13, 2019
Wingu la simanzi limetanda katika kijiji cha Sisokhe eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega nchini Kenya  baada ya mwalimu mkuu aliyekuwa ameenda kwa mganga wa jadi kufariki dunia katika mazingira tatanishi.

Vivian Atuvuka aliaga dunia Jumatatu Machi 11,2019 muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwa mganga huyo ambaye anadaiwa kumtenga kwenye chumba kimoja kando na wateja wengine. 

Inaelezwa kuwa Vivian Atuvuka anasemekana kugombana na jirani yake kuhusu mpaka wa shamba hivyo basi, alifika kwa Mganga huyo wa jadi kwa ajili ya kupata msaada kutoka kwa mganga jinsi angekabiliana na jirani huyo.

Inaarifiwa kuwa mganga Beatrice Okumu alimkuta Atuvuka akiwa ameshafariki dunia wakati wake wa kumhudumia ulipowadia.

 Mwalimu huyo alitaka ushauri kutoka kwa mganga jinsi angekabiliana na jirani wake kuhusu mzozo wa mpaka wa shamba.

"Alilalamika kuhusu maumivu ya kichwa na akanywa pakiti ya maziwa aliyokuwa nayo kwenye mkoba wake akisubiri kuhudumiwa," Dismas Okum ambaye ni mumewe mganga huyo alisema.

 Mhudumu wa boda boda aliyempeleka Atuvuka kwa mganga huyo alisema alikuwa mchangamfu sana na hakuonyesha dalili zozote za kuwa mgonjwa.

Kulingana na mhudumu huyo wa boda boda, mwalimu huyo amekuwa akizozana na jirani wake kuhusu mpaka wa shamba kwa muda mrefu. 

Mmoja wa jamaa zake naye alisema mwalimu huyo hakuwa anaugua sana alipotoka nyumbani ila alikuwa amelalama kuhusu maumivu kwenye mkono wake wa kulia. 

Maafisa wa polisi wamemkamata mganga huyo ili aweze kusaidia katika uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwalimu huyo. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post