JAMAA APOTEZA UUME BAADA YA KUJIKUNA

Jamaa aitwaye Fredrick Ochieng'  wa nchini Kenya ana matumaini kuwa siku moja afya yake ya kawaida itarejea licha ya kwamba amepoteza uume wake kwa miaka tisa sasa. 

Ochieng' anasema alikuwa buheri wa afya hadi mwaka wa 2010 alipoanza kuhisi kujikuna katika sehemu nyeti kila mara. 

 Lynn Ngugu, Ochieng' ambaye alifiwa na mkewe miaka kadhaa iliyopita, anasema  amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja kule Muhoroni ila hajawahi kupata nafuu. 

" Nilianza kujikuna kwenye sehemu nyeti, kisha nikawa na kidonda kilichochipuka na kusababisha uume wangu kukatika," Ochieng', alisema.

Ochieng' alisema madaktari wameshindwa kubaini anaugua ugonjwa upi ila kwa mara ya kwanza walidhani ulikuwa ugonjwa wa saratani. 

Kwa sasa Ochieng' hana uume wake ila anatamani sana aoe tena, apate mke ambaye atampikia, amfulie na atunze watoto wake bila kutaka kushiriki ngono. 

Hata hivyo mamaake anasema itakuwa vigumu kwa mwanawe kupata mke kwani hawezi akamtosheleza kingono. 

 Ochieng' alisema jamaa zake wanajiweza kifedha lakini wamemtelekeza hata hawajali jinsi anavyougua.

 "Jamaa zangu wanajiweza kifedha na kila ninapowaomba msaada, wananiambia eti niwache kuwasumbua, ugonjwa huu umenitesa sana , hata kwa sasa sina uume," Ochieng; alielezea. 

Kwa sasa anataka wasamaria wema kumsaidia kuchanga KSh 100,000 ili apate matibabu spesheli.

Via Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527