WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE

Washindi wa Televisheni katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na  ushinde wakiwa na zawadi zao muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa wakati  wa hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite Bottlers mjini  Moshi 
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers mkoa wa Arusha,Boniface Mwase akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde walijinyakulia Televisheni. 
 Baadhi ya Washindi wa Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde wakimsikiliza Meneja Mauzo wa Kampuni ya vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers mkoa wa Arusha,Boniface Mwase wakati akitangaza majina ya washindi wa Televeisheni wakat wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite.
Mratibu wa Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Leonard Makuka akikabidhi zawadi ya Televeisheni kwa Hadija Mmbughu ,mshindi katika promsheni ya Coke Studio kunywa na ushinde. 
Mtathimini wa Biashara katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite  Bottlers ,Japin Solank akikabidhi zawadi ya Televisheni kwa Mshindi  katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde ,Mohamed Hussein  ,mkazi wa Pasu mjini Moshi. 
Mratibu wa Mauzo katika kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers ,Godfrey Amani akikabidhi zawadi ya Televisheni kwa mshindi wa  Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde ,Laurant Mlingi mkazi wa Arusha. 
Baadhi ya zawadi za Televeisheini zilizotolewa kwa washindi. 
Washindi wa Televisheni katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na  ushinde wakiwa na zawadi zao muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa wakati  wa hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite Bottlers mjini  Moshi 
Washindi wa Televisheni katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na  ushinde wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho kujionea uzalishaji unavyofanyika. 
Sehemu ya kiwanda cha kuzalisha vinywaji baridi jamii ya Cocacola ,kiwanda cha Bonite Ltd mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .


ZAIDI ya wateja 15,000 wa vinywaji baridi vinavyozalishwa na kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mjini Moshi wamejishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya “Coke Studio kunywa na Ushinde “ inayoendelea .


Wateja hao wamejishindia zawadi baada ya kununua soda jamii ya Cocacola ,Fanta na Sprite zikiwa katika ujazo wa mililita 350 na mililita 500 huku wengine 22 wakikabidhiziwa zawadi zao za Televisheni za kisasa za ukubwa wa inchi 32.

Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao kutoka mikoa ya ,Arusha,Kilimanjaro na Manyara imefanyika katika viunga vya Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd na baadae washindi wote walipata nafasi ya kutembelea na kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za Bonite.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Boniface Mwase alisema wateja wa bidhaa zinazozalishwa na Bonite kila mmoja yupo kwenye nafasi ya kujishindia
zawadi kwa kutumia kiasi cha Sh 500 na sh 1000.

“Zawadi ambazo tumezitoa leo ni televisheni 22 kwa washindi ambao wamejitokeza ,zipo zawadi za soda za bure ,zipo zawadi za fedha kiasi cha sh 5000 hadi 10,000,hizi zinatolewa pamoja hapo mteja anapokunywa soda anashinda
papo hapo “,alisema Mwase.


Alisema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye shindano la Coke Studio kunywa na ushinde na washindi wameendelea kupatikana kutoka maeneo yote ambayo bidhaa
za Bonite zinapatikana na kwamba kila atakayeshinda atafikishiwa zawadi yake kwa wakati.

Mwase alisema Bonite imekuwa na utaratibu wa kufanya Promosheni kila mara lengo likiwa ni kurejesha sehemu ya faida inayopata kwa wateja ambao wamekuwa wakiunga mkono kampuni hiyo kwa kutumia bidhaa zake.

“Nitoe wito kwa wateja wetu waendelee kutumia soda za jamii ya Coca Cola kwa sababu zawadi bado ni nyingi na kila mmoja ana nafasi ya kushinda.”alisema Mwase.


Zainaabu Lusoke ,mkazi wa Arusha ni mmoja wa washindi wa Televisheni katika promoshen ya Coke Studio kunywa na ushinde amesema zawadi hiyo inatokana na Mama yake mdogo aliyemtaka kuokota kizibo alichotupa pindi
aliponunua Soda aina ya Fanta.

“Katika shindano hili sikutegemea kama nitashinda ,nilinunua soda nikatupa kile kizibo ,ma mdogo akaniambia kwa nini unatupa ,nikamwambia hivi vizibo vya Bonite
vimeandikwa Jaribu tena ,akaniambia kachukue kile kizibo ,ndipo nilipotizama nikakuta nimeshinda TV”,alisema Zainabu.

Washindi waliojinyakulia zawadi za Televisheni ni pamoja na
Mariam Mkara,Saumu Rashid ,Hadija Mmbughu,Emanuel Magige,Lightnes Lusega,Mwanahawa Miraji,Mohamed Hussein na Fadhili Lyimo.

Wengine ni Hilda Silayo,Judith Assey ,Haruna Mohamed,Nasibu Juma,Happy Kombe,Fii Mkwanda,Emanuel John,Nembris Simon,Godfrey Wilson ,Zainabu Salim,Rajabu Miraji,Said Massatu na Laurant Mlingi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527