SERIKALI YATANGAZA KUANZA KUTOA CHAI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA CHEKECHEA NA MSINGI


Chakula cha subuhi
Wizara ya Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijijini ya Botswana imetangaza kuanza kutoa chakula cha asubuhi kwa wanafunzi wa shule za chekechea na shule za msingi nchini humo kuanzia mwezi ujao.

Tangazo hilo ambalo limeelezwa kuwa ni la haraka, limetolewa Machi 18 ambapo linasema kuwa wanafunzi hao wataanza kupewa bure chakula cha asubuhi kuanzia April Mosi kwaajili ya mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Serikali ya Botswana imefikia uamuzi huo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na timu iliyoundwa mwaka 2013 kuwa wanafunzi wanatakiwa kupewa vyakula vyenye virutubisho ili kulinda afya zao, ukuaji na maendeleo pamoja na kupunguza magonjwa yatokanayo na upungufu wa lishe bora.

Chakula ambacho kinatarajia kutolewa ni pamoja na chai, mkate, 'peanut butter', mayai yaliyochemshwa, uji, maziwa, machungwa na 'apple'.

Chakula hicho kimependekezwa kutokana na mahitaji ya virutubisho kwa wanafunzi, ambapo kitatolewa kwa wanafunzi hao kila siku asubuhi kabla ya kuanza masomo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527