ALIYEMSHIKA 'MAKALIO' GADIEL AADHIBIWA


Kushoto ni Juma Nyangi na kulia ni Gadiel Michael

Klabu ya soka ya Alliance FC, ya jijini Mwanza imemwadhibu mchezaji wake Juma Nyangi kwa kitendo chake cha kumshika makaliko mchezaji wa Yanga Gadiel Michael katika mchezo wa ligi kuu, Machi 2, 2019.

Akiongea leo baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Alliance, Yusuph Budodi amesema wameamua kumkata mshahara.

''Kamati imetazama kwa kina na kuamua kutompa mshahara wa mwezi mmoja ili iwe fundisho kwa wengine na kwasababu amekiri hatukuona kama ni vyema kumsimamisha mechi au vinginevyo lakini kukosa mshahara pia ni jambo kubwa'', amesema.

Awali Juma Nyangi aliitwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo na kuhojiwa kabla ya kamati hiyo kufikia maamuzi.

Kwa upande wake Juma Nyangi, amesema ameumizwa na adhabu hiyo na hatorudia tena huku akiweka wazi kuwa hakukusudia kufanya hivyo ila ilitokea kwasababu ya presha ya mchezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post