WEZI SUGU WATATU WAPEWA ZAWADI YA VALENTINE DAY


Wezi watatu sugu ambao wamekuwa wakiwahangaisha watu katika eneo la Barnabas, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya wameteketezwa moto hadi kufa Siku ya Wapendanao "Valentine Day", Februari 14,2019.

 Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, washukiwa hao walikiri mbele ya umma kuhusika katika matukio mbali ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo na kuwakosesha wenyeji amani.

 Kulingana na Joseph Maina ambaye ni mkazi, aliyezungumza na Taifa Leo, Alhamisi, Februari 14 wahalifu hao wamekuwa wakihangaisha raia kwa muda mrefu sana.

 Polisi walifika baadaye na kuichukua miili yao baada ya waliokuwa wakishuhudia kusababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi.

“Hii sio mara ya kwanza kupata tabu mikononi mwa wahalifu, wanaotekeleza maovu peupe bila kuogopa idara ya usalama,” alisema. 

Bw Maina alisifia hatua ya wananchi kuangamiza sehemu ya genge hilo kwani vyombo vya usalama vimekuwa vikishindwa kutoa msaada kwao.

Imeelezwa kuwa, wahudumu wa boda boda pia walieleza kuwa shida ambazo wamekuwa wakipitia, zimechangiwa sana na majambazi hao kwani huwashambulia kila mara na kuwanyang’anya pikipiki zao na huwa wamejihami kwa silaha hasa nyakati za usiku.

Wakazi wafika kwa wingi kushuhudia wezi watatu walioteketezwa moto hadi kufa katika eneo la Barnabas, Kaunti ya Nakuru. 

 Itakumbukwa siku chache zilizopita, mwendeshaji mmoja wa boda boda aliuawa katika hali ya kutatanisha na inasadikiwa waliouawa ni sehemu ya genge la majambazi waliohusika na mauaji hayo.

 Wananchi walifika kwa wingi kushuhudia tukio hilo na waliwalaumu sana pilisi na wamiliki wa maeneo ya burudani kwa ongezeko la uhuni eneo hiulo. 

 Kamanda wa Polisi (OCPD) Kaunti ya Nakuru Samwel Obara hakufika kwa wakati ili kutoa taarifa yake kuhusiana na mauaji hayo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527