PESA ZA MBUNGE ROSE TWEVE ZAGEUKA LULU KWA AKINA MAMA WA KATA YA NZIHI IRINGA



Baadhi ya wajumbe wa kikundi cha Rose Tweve kilichopo kata ya Nzihi mkoaniri Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kikao chao cha kikatiba
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameendelea kuitunisha mifuko ya wanawake wa UWT mkoa wa Iringa kwa kukuza mtaji walipewa awali na mbunge huyo.

Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa kikundi cha Rose Tweve, Aulelia Mbembe amesema mbunge wa viti maalum Rose Tweve aliwapa mtaji wa shilingi laki tano(500,000/=) kwa kuanzia lakini waliunda kikundi na kukiita Rose Tweve kwa lengo la kumuuezi mbunge huyo kwa mchango wake kwa wanawake wa UWT kata ya Nzihi mkoani Iringa.

“Mbunge alitupa mtaji lakini tulijiongeza kwa kukopeshana kwa riba ndogo ambayo tulijipangia sisi wenyewe kwa kukopeshana na kukutana kwa mwezi mara moja kwa ajili ya kununua hisa pamoja na kubadilisha mawazo kwa lengo la kukuza mitaji na kufanya maendeleo yetu binafsi” ,alisema Mbembe. 

Mbembe alisema mtaji wa kikundi cha Rose Tweve kimefanikiwa kukuza mtaji kutoka shilingi laki tano 500,000/=) hadi kufikia kiasi cha shilingi milioni kumi laki moja na nusu (10,150,000/=) kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka mwaka 2017 hadi hii leo hapo ndio utajua kuwa ukimwezesha mwanamke unakuwa umeikomboa jamii.

‘’Kama kikundi tunategemea kuja kuwa na miradi yetu mikubwa itakayokuwa inaingiza faida kwetu na taifa kwa ujumla kupitia kulipa kodi kwa miradi hiyo ,lakini tunategemea kutembelea na kusaidia vikundi vya watu maalumu kama vile walemavu ,yatima ,wazee wasiojiweza,na waathirika wa vvu,yote haya ni mchango na matunda ya Mbunge Rose Tweve ,kwa kweli shukrani nyingi zifike kwake ,na viongozi wengine wachukue mfano wa mbunge dada Rose Tweve kwa kusaidia jamii kama Rose Tweve alivyotusaidia sisi kikundi cha akiba cha wanawake(UWT) Rose Tweve Nzihi”, alisema Aulilelia Mbembe mwenyekiti wa kikundi hicho.

“Hebu angalia ndugu mwandishi wa habari jinsi gani wanawake wa UWT kata ya Nzihi tulivyoweza kutumia vizuri fursa tuliyoipata kutoka kwa mbunge Rose Tweve kwa kutusaidia kubadilisha maisha yetu kwa kuweza kujikimu kimaisha tofauti na ilivyokuwa hapo awali hivyo tunamshukuru sana mbunge Rose Tweve”, alisema Mbembe.

Mery Msigara ni moja wa wajumbe wa kikundi cha akiba cha Rose Tweve alisema kuwa alikuwa anashinda nyumbani kwa kumtegemea mume wake kwa kila kitu lakini baada ya kujiunga kwenye kikukidi cha Rose Tweve amekuwa mjasiriamali anayeweza kufanya biashara ndogondogo na kupata faida kila kukicha huku familia yake ikipata maendeleo ukilinganisha na awali,yote haya ni matunda ya mbunge Rose Tweve.

Wajumbe katika kikundi hicho wameonekana kuwa na malengo makubwa katika kufanikiwa huku wakisema kwa mwanga waliooneshwa na mbunge Rose Tweve wanaamini watafikia malengo yao ya mbali kimafanikio kupitia kikundi hicho cha akiba cha Rose Tweve .

Hadi sasa mbunge Rose Tweve amefakiwa kuvifikia na kuvitembea jumla ya vikundi 92 vya mkoani iringa na kuviwezesha kama ilivyo kwa hiki kikundi cha kata ya Nzihi. 


Na Fredy Mgunda - Iringa 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527