HIKI NDICHO WANACHO KIWAZA WANAUME WENGI KUHUSU KUINGIA KATIKA MAHUSIANO /NDOA NA SINGLE MOTHER

Wewe ni Single Mother ? Upo katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ? Au unataka kuingia katika mahusiano ya kimapenzi/uchumba/ndoa na mwanaume ambae si baba wa mtoto wako?

Basi kabla ya kufanya hivyo,unatakiwa kujua kitu gani wanacho kiwaza wanaume wanao ingia katika mahusiano na single mothers.
Pia unatakiwa kuyafahamu mambo wanayo yawaza wanaume wengi kabla ya kuingia katika ndoa na single mothers.

Mahusiano mengi ya single mothers yanashindwa kufika mbali kwa sababu single mothers wengi huwa wanaingia katika mahusiano na wanaume bila kuyafanyia analysis mambo haya muhimu kabisa kwa kila single mother kuyafahamu.

AFRICANDADAZ imekusanya maoni kutoka kwa wanaume mbalimbali kuhusu uzoefu wao na mtazamo wao kuhusu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa na single mothers.

 Maoni haya yamechukuliwa kutoka kwa wanaume mbalimbali wa hapa Tanzania na waliopo nje ya Tanzania.

 Baadhi ya mambo yanayosemwa na wanaume hawa kuhusu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa na single mothers yanatisha na kuogofya sana. 

 Ni vyema kila single mother ambaye anafikiria kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au kuingia katika ndoa na mwanaume ambae si baba wa mtoto wake ayafahamu mambo haya.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka kundi la wanaume ambao wanafanya kampeni ya unyanyapaa dhidi ya single mothers na kuwafanya waonekane kama wanawake ambao hawastahili kupendwa tena au kama wanawake ambao hutakiwi kuingia nao katika ndoa. 

 Mara kwa mara katika mitandao mbalimbali ya kijamii zimekuwa zikiibuliwa mada zenye lengo la kuwashushia hadhi single mothers.

Baadhi ya single mother kama sio wote wamekuwa wakikerwa na kukatishwa tama sana na maneno hayo ya hovyo kuhusu single mothers  kwani kusema ukweli maneno hayo ni maneno yanayo kera sana ambayo si kila single mother anaweza kuyavumilia.

Kibaya zaidi wakati mwingine suala la unyanyapaa dhidi ya single mothers huingia katika level ya kifamilia. 

 Yaani unakuta binti ananyanyapaliwa na wanafamilia yake kwa sababu amejifungua akiwa nyumbani.

 Baadhi ya mabinti hawa huwa wanashindwa kuvumilia na wengine hufikia hatua ya kutaka kujiua.

Kama hiyo haitoshi, baadhi ya familia kijana wao anapo taka kufunga ndoa na single mother wazazi wamekuwa wakiingilia kati na kumuonya kijana wao asithubutu kumuoa single mother. 

Hali hii imekuwa ikiwatisha na kuwaogopesha single mothers wengi na matokeo yake wengi wao wamejikuta wakiwa wanaingia katika mahusiano na mwanaume yoyote tu ili kujisitiri.

Kibaya zaidi ni pale mwanaume huyo anakuwa na mentality kwamba “ Single mother don’t have any other option “ kwani kitakacho endelea hapo ni mateso na manyanyaso mazito sana ambayo single mother huyu hawezi kuyavumilia. 

Single mother huyu anaposhindwa kuvumilia mateso na manyanyaso ya mwanaume huyu, huamua kuondoka kwa mwanaume huyo na kuendelea na maisha yake mengine.

Mwanaume huyu kwa sababu ya uchungu wa kuachwa na mwanamke, anaanza kutoa maneno ya kashfa kuhusu single mothers.

 Asilimia kubwa ya wanaume hao ndio hawa tunao waona kwenye mitandao ya kijamii wakitoa maneno ya kashfa na unyanyapaa dhidi ya single mothers kwa kuwafanya waonekane hawana maana.

USHAURI WANGU KWA SINGLE MOTHERS: Usikatishwe tama na maneno ya kashfa ya wanaume na usikubali kuteswa na kunyanyaswa na mwanaume kwa sababu eti anajua wewe ni single mother kwamba anafikiri hauna option.

Kingine usikubali kuingia katika mahusiano na mwanaume wa hovyo kwa sababu tu wewe ni single mother.

Muhimu: Jua kile wanacho kiwaza wanaume kuhusu kuwa katika mahusiano au ndoa na single mother.

 Ukijua hili itakusaidia sana kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia katika mahusiano au ndoa na mwanaume ambae sio baba wa mtoto wako.

Kusoma zaidi makala haya tembelea Kwa kubofya hapo chini :

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527